Swali: Mke wangu anaishi pamoja nami Saudi na anataka kuwatumia mzazi wake picha wanaoishi Misri ili apate utulivu. Na nimesikia Fatwa kuwa picha kwa ala ya picha ni Haramu. Je, hii ni dharurah?

Jibu: Hii sio dharurah. Haifai kwake kutuma picha yake, sawa kwa mama yake wala asiyekuwa mama yake. Kwani hii sio dharurah. Amuandikie [barua], aongee nae kwenye simu. Alhamduli Allaah. Ama kutuma picha haijuzu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb
  • Imechapishwa: 30/03/2018