Je, mwanafunzi ataje tofauti za wanachuoni?

Swali: Mwanafunzi anatakiwa kushika msimamo gani juu ya tofauti yenye kuzingatiwa? Je, watu walazimishwe maoni ya mwanachuoni mmoja au ni katika amana ya kielimu kutaja ile tofauti na kumwelekeza katika maoni ambayo yeye anaona kuwa ndio yenye nguvu zaidi?

Jibu: Kama anazungumza na wanafunzi awatajie tofauti na dalili na awabainishie yale maoni ambayo anaona kuwa na nguvu zaidi.

Ama kama inahusiana na fatwa mtu hapaswi kumtajia yule anayemjibu maoni mbalimbali. Katika hali hii amtajie maoni anayoona kuwa na nguvu zaidi kwa dalili.

Kwa hiyo kuna kuzungumza na kuwafunza wanafunzi. Hapa kunatajwa tofauti na dalili na kunabainishwa maoni sahihi zaidi kwa dalili.

Lakini inapokuja kwenye fatwa, asiwachanganye watu kwa kuwatajia tofauti. Katika hali hii anatakiwa kubainisha maoni yenye nguvu zaidi kwa dalili. Ni jambo linalojulikana kwamba mtu anayetoa fatwa anatoa jibu la sawa. Hata hivyo haipelekei kwamba ni lazima ifuatwe. Ama hukumu inatakiwa kubainishwa na ni lazima kuifuata.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=137119
  • Imechapishwa: 30/06/2019