Swali 191: Salafiyyah ni pote katika mapote? Je, mtu anasemwa vibaya kwa kujinasibisha nalo?

Jibu: Salafiyyah ndio kundi lililookoka. Nao ndio Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Sio pote miongoni mwa mapote ambayo yanaitwa Ahzaab. Ni kundi lililo juu ya Sunnah na juu ya dini. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Halitoacha kundi kutoka katika Ummah wangu kuwa ni lenye kushinda. Halitodhurika na wale wenye kuwakosesha nusura na wale wenye kwenda kinyume nao.”

“Ummah wangu utafarikiana katika mapote sabini na mbili. Yote yataingia Motoni isipokuwa moja.” Wakasema: “Ni lipi hilo, ee Mtume wa Allaah?” Akasema: “Ni wale watakaokuwa juu ya mfano wa yale niliyomo mimi hii leo na Maswahabah zangu.”

Salafiyyah ni kundi linalofuata yale aliyokuwemo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake. Sio pote kama yalivyo mapote mengine hii leo. Ni kundi ambalo athari yake ni ya tangu hapo kale kuanzia wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo baadaye likarithiana na kuendelea. Halitoacha kuwa juu ya haki hali ya kushinda mpaka Qiyaamah kisimame, kama alivoeleza (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ´Ulamaa-ul-Kibaar fiy al-Irhaab wat-Tadmiyr, uk. 404
  • Imechapishwa: 03/03/2020