Swali: Je, njia za Da´wah zimejengeka chini ya msingi wa Qur-aan na Sunnah au ni masuala ya Ijtihaad? Kwa mfano inafaa kwetu kucheza mpiga ili kuwavutia vijana katika Uislamu?

Jibu: Sionelei kuwa njia hizi zinajuzu kuzichukulia kuwa ni njia za Da´wah na hivyo kwa kuwa baadhi yazo ni upuuzi (michezo). Isitoshe imepokelewa Hadiyth ya Mtume na Imaam Nasaa´iy kwenye “as-Sunan al-Kubraa” kutoka kwa Jaabir bin ´Abdillaah al-Answaariy kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema:

“Michezo yote anayojishughulisha nayo binaadamu ni upuuzi; isipokuwa kucheza na mke wako, kufanya mazoezi na farasi yako, kupiga mshale na kuogelea.”

Haya ni mambo mane aliyotaja Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwa si katika michezo ya kipuuzi. Michezo mingine yote ambayo mtu anajishughulisha nayo ni ya kipuuzi (batili) isipokuwa haya mambo mane.Tukija katika michezo ambayo imejitokeza siku hizi; kama mchezo wa mpira wa mikono kama ilivyokuja katika swali, yatosheleza kuruhusu kwa makusudio ya Kishari´ah nayo ni kujengwa mwili. Ama kuchukuliwa kuwa ni katika njia za Da´wah, kwanza ni jambo jipya katika Uislamu. Halijulikani na Waislamu karne zote hizi zilizopita kuwa walikuwa wakitumia upuuzi, hata ikiwa unajuzu, kuwa ni katika njia ya Da´wah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawa Juddah (16 B)
  • Imechapishwa: 09/04/2022