Swali: Je, matapishi ni najisi? Je, yanachengua wudhuu´?

Jibu: Kinachojulikana kwa wanachuoni ni kwamba matapishi yakiwa mengi ni najisi na hukumu yake ni kama mkojo na yanatakiwa kuoshwa. Kuhusu kwamba yanachengua wudhuu´ ni jambo lina maoni tofauti. Ama yakiwa ni madogo tu hayachengui wudhuu´. Maoni yenye nguvu ni kwamba akijitapikisha basi atatakiwa kutawadha. Ama matapishi yakimshinda na akajaribu kuyazuia, asitawadhe. Mfano wake ni kama funga. Mfungaji akiyazuia matapishi basi swawm yake ni sahihi. Ama akijitapikisha basi atatakiwa kuilipa siku hiyo. Haya ndio maoni yenye nguvu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (10) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191426#219753
  • Imechapishwa: 14/05/2019