Je, mali ya haramu inaingia katika vitu vya kurithi?

Swali: Kuna mtu alikuwa anafanya biashara ya haramu ambapo akapata mali nyingi. Baadaye mtu huyo akafa. Je, inafaa kwa warithi wake wakatumia mali hii na wakaigawanya kati yao?

Jibu: Ndio. Iwapo mtu alikuwa akichuma mali kwa njia ya haramu kisha akafariki, mali hii ni halali kwa warithi wake na madhambi ni kwa yule maiti. Isipokuwa tu ikiwa kama warithi watajua kwamba ni ya mtu maalum, katika hali hiyo ni wajibu kwao kumridhia nayo. Mfano wa hilo mtu alimdhulumu mtu mwingine ardhi na akavuka mipaka, kisha mtu huyo akafa. Warithi wanatambua kuwa ardhi hii ni ya jirani yao. Basi ni wajibu kwao kuirudisha kwa jirani yao. Kwa sababu hii ni mali yake maalum. Mfano mwingine kama ataiba kitu na pesa hiyo akabaki nayo kisha akafa, basi ni wajibu kwa warithi wake kurudisha pesa hii kwa mwenye nayo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (57) http://binothaimeen.net/content/1304
  • Imechapishwa: 22/10/2019