Swali: Je, kutokwa na madhiy kunalazimisha kuoga?

Jibu: Kutokwa na madhiy hakulazimishi kuoga. Lakini kunawajibisha kutawadha baada ya kuosha uume na uke anapotaka kuswali, kutufu au kugusa msahafu. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipoulizwa juu yake alisema kuwa mtu anatakiwa kutawadha na akamwamrisha aliyepatwa na madhiy aoshe uume na uke wake. Kinacholazimisha kuoga ni manii pindi yanapotoka kwa kasi na kwa kuhisi ladha au akaona athari yake baada ya kuamka kwake kutoka usingizini mwake mchana au usiku.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/187)
  • Imechapishwa: 28/08/2021