Je, kutokwa na damu puani kunachengua wudhuu´?


Swali 04: Je, kutokwa na damu puani kunachengua wudhuu´?

Jibu: Kutokwa na damu puani hakuchengui wudhuu´. Hakuna dalili juu ya kwamba kunachengua wudhuu´. Kumepokelewa Hadiyth dhaifu inayosema kuwa kunachengua. Lakini hata hivyo haikuthibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) walikuwa wakiswali na majeraha yao. Kwa hivyo hakuchengui. Lakini Lakini akichelea kuchafua msikiti basi atoke nje na aoshe arudi na ajengee juu ya swalah yake.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ijaabatu as-Saa-il, uk. 32
  • Imechapishwa: 22/09/2019