Je, kuna tofauti kati ya shirki na kufuru?


Swali: Je, kuna tofauti kati ya shirki na kufuru?

Jibu: Ndio, kufuru ni yenye kuenea zaidi kuliko shirki. Kafiri anaweza kuwa mwenye kumkanusha Mola (Subhaanahu wa Ta´ala). Si mwenye kumuamini Mola kama mfano wa Fir´awn, Mu´attwilah na Dahriyyah. Kuhusu mshirikina ni mwenye kumuamini Mola. Lakini hata hivyo anashirikisha pamoja Naye wengine. Kati ya shirki na kufuru kuna mambo yenye kuenea na mambo maalum.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 32
  • Imechapishwa: 11/05/2018