Je, inasihi kuswali Witr mkusanyiko pamoja na kunitajia dalili?

Swali 29: Je, inasihi kuswali Witr mkusanyiko pamoja na kunitajia dalili?

Jibu: Inasihi. Mara nyingi katika matendo ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kwamba alikuwa anaswali peke yake. Lakini (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwahi kuswali na ´Abdullaah bin ´Abbaas akasimama pamoja naye – kama ilivyopokelewa na al-Bukhaariy na Muslim kutoka katika Hadiyth ya ´Abdullaah bin ´Abbaas – na akataka kusimama upande wa kushoto wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo akamvuta upande wake wa kulia. Hii ni dalili ya kujuzu.

Kisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) usiku mmoja wa Ramadhaan aliswali peke yake ambapo Maswahabah wakamuona na wakaswali swalah yake. Kisha usiku wa pili na wa tatu wakawa wengi zaidi. Baadaye akaacha. Haya yamepokelewa na al-Bukhaariy na Muslim. Vilevile imepokelewa katika “al-Jaamiy´” ya at-Tirmidhiy kupitia kwa Abu Dharr ya kwamba usiku mmoja Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliswali pamoja naye ambapo akasema: “Ee Mtume wa Allaah! Lau ungetuzidishia?” Ndipo akasema:

“Hakika yule atakayeswali pamoja na imamu basi huandikiwa ameswali usiku mzima.”

Kisha akawaswalisha usiku wa pili na akawaswalisha mpaka akasema:

“Nimechelea tusipitwe na al-Falaah.” Akasema: “Mnajua nini al-Falaah?” Akasema: “Ni daku.”

Hii ni dalili inayoonyesha kuwa inafaa kuswali swalah ya Sunnah mkusanyiko. Lakini, ndugu zanguni, haikuwa ni mazowea ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiiswali mkusanyiko. Kwa hivyo haitakikani iwe ndio mazowea ya mtu. Lakini ni sawa endapo atafanya hivo katika baadhi ya nyakati. Endapo ataswali peke yake basi ndio bora zaidi – Allaah akitaka.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ijaabatu as-Saa-il, uk. 76
  • Imechapishwa: 25/09/2019