Je, inajuzu mwanamke kuvaa suruwali pana isiyobana?


Swali: Ipi hukumu ya kuvaa suruwali kwa mwanamke? Na je, kuna tofauti ikiwa pana au nyembamba?

Jibu: Katika mji wetu si ada ya wanawake kuvaa suruwali, na wanawake wanavaa kutokana na wavaavyo wanawake wa mji. Haijuzu khaswa kayika mji huu [Saudi Arabia] kuvaa suruwali. Hata katika miji mingine, kwa kuwa suruwali inabainisha mwili wa mwanamke wala haisitiri stara kamili. Na huenda fitina ya suruwali ikawa kubwa. Kwa kuwa inadhihirisha yaliyomo ndani. Mwanamke ajiepushe kuvaa suruwali, hususan katika mji huu kwa kuwa hii si katika ada ya mji huu. Mwenye kuvaa mavazi yanayokwenda kinyume na makubaliano [ya waislamu] basi yuko katika makemeo makali [kwa Mola Wake].

Swali: Vipi akivaa yuko nyumbani?

Jibu: Hata nyumbanni [haijuzu]. Kwa kuwa ataanza kuivaa nyumbani kisha hatua baada ya hatua ataanza kuivaa hata barabarani.

  • Mhusika: ´Allaamah Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.youtube.com/watch?v=165rIMROtGY
  • Imechapishwa: 07/09/2020