Je, inajuzu kukusanya picha kwa lengo la ukumbusho?

Swali: Je, inajuzu kukusanya picha kwa lengo la ukumbusho?

Jibu: Haijuzu kwa muislamu yeyote, wa kiume au wa kike, kukusanya picha kwa lengo la ukumbusho. Nakusudia picha za viumbe wenye roho za mwanadamu au kiumbe chenginecho. Bali ni lazima kuiharibu. Hayo ni kutokana na yale yaliyothibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye alimwambia ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh):

“Usiache picha hata moja isipokuwa umeiharibu wala kaburi lililoinuka isipokuwa umelisawazisha.”[1]

Vivyo hivyo imethibiti kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba amekataz picha nyumbani. Wakati alipoingia Ka´bah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) siku ya ufunguzi aliona ukutani mwake picha ambapo akaomba maji na kinguo na akaifuta.

Kuhusu picha za viumbe visivyokuwa na uhai kama vile mlima, mti na mfano wake hazina ubaya wowote.

[1] Muslim (969).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (04/225) https://binbaz.org.sa/fatwas/864/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%AC%D9%85%D8%B9-%D8%A7%D9%84%D8%B5%D9%88%D8%B1-%D8%A8%D9%82%D8%B5%D8%AF-%D8%A7%D9%84%D8%B0%D9%83%D8%B1%D9%89
  • Imechapishwa: 03/12/2019