Je, inafaa mwanamke kujipamba kwa kutia wanja kwenye macho yake?


Swali: Je, inafaa mwanamke kujipamba kwa kutia wanja kwenye macho yake?

Jibu: Inafaa kwa mwanamke kujipamba kwa kuweka wanja machoni mwake akiwa kati ya wanawake, mbele ya mume na Mahaarim zake. Akiwa mbele ya wanamme wa kando haijuzu kwake kufunua uso wake wala macho yake yaliyotiwa wanja. Amesema (Subhaanah):

وَإِذَا سَأَلْتُمُوهُنَّ مَتَاعًا فَاسْأَلُوهُنَّ مِن وَرَاءِ حِجَابٍ

“Mnapowauliza haja, basi waulizeni nyuma ya pazia.”[1]

Hapana neno kutumia Burqu´ inayoonyesha macho mawili au jicho moja. Lakini afanye hivo pasi na kuweka wanja mbele ya wanamme ambao ni kando naye.

Makusudio ya wanamme wa kando ni wale ambao sio Mahram zake kama mfano wa kaka wa mumewe, mjomba wa mumewe, binamu zake upande wa baba wakubwa na baba wadogo na upande wa mashangaz na mfano wa watu hao. Ni mamoja watu hao ni waislamu au makafiri.

[1] 33:53

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/57)
  • Imechapishwa: 08/08/2021