Je, inafaa kwa mwanamke kutia nywele zake rangi nyeusi?


Swali: Je, inafaa kwa mwanamke kutia nywele zake rangi nyeusi?

Jibu: Haijuzu kwa mwanamke wala mwengine kuzibadilisha mvi kwa rangi nyeusi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Zibadilisheni mvi hizi na epukeni rangi nyeusi.”

Ameipokea Muslim katika “as-Swahiyh” yake.

Lakini hapana neno kuzibadilisha kwa rangi nyingine isiyokuwa nyeusi. Pia hapana neno kuzibadilisha kwa rangi ya hina au katam iliyochanganywa muda wa kuwa rangi haitojitokeza nyeusi na badala yake ijitokeza kati ya nyeusi na nyekundu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/53)
  • Imechapishwa: 08/08/2021