Je, inafaa kwa muislamu kumrithi ndugu yake ambaye haswali?


Swali: Je, inafaa kwa muislamu kumrithi ndugu yake ambaye haswali? Je, amswalie?

Jibu: Hapana. Mwenye kuacha swalah kwa kukusudia kwa mujibu wa maoni yanayosema kuwa ni kafiri – nayo ndio maoni yenye nguvu – anataamiliwa matangamano kama makafiri wengine. Hivyo haoshwi, havikwi sanda, haswaliwi, hazikwi sehemu ya makaburi ya waislamu na wala harithiwi. Hatorithiwa na makafiri wala waislamu. Mali yake inatakiwa kuchukuliwa na ifanywe kuwa fai katika hazina ya waislamu. Hii ni kama mali iliopotea isiyokuwa na mmiliki na iwekwe katika hazina ya waislamu. Hii ndio hukumu yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam http://ajurry.com/safrawy/chorohat-elakida/chorohat-nawakid-elislam/charh-salah-fawzan/03.mp3
  • Imechapishwa: 12/10/2018