Je, inafaa kuchukua malipo kwa ajili ya kufunza Qur-aan?

Swali: Je, inafaa kuchukua malipo kwa ajili ya kufunza Qur-aan?

Jibu: Ndio, hakuna neno. Imethibiti katika “as-Swahiyh” ya al-Bukhaariy ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika kilicho na haki zaidi ya kuchukuliwa malipo ni Kitabu cha Allaah.”

Jengine ni kwa sababu mtu anaweza kutenga muda wake kwa ajili ya kufunza na akajishughulisha badala ya kutafuta chumo lake yeye na watoto wake.

Kilichokatazwa ni mtu kuchukua malipo kwa ajili ya kisomo chenyewe. Jambo hili limekatazwa na halifai. Kuna tofauti kati ya kuchukua malipo juu ya kufunza na kuchukua malipo juu ya kisomo. Baadhi ya watu wanaalika watu waje kuwasomea Qur-aan na kisha anampa pesa juu ya kile kisomo au kwa ajili amemsomea maiti. Kitendo hichi hakijuzu. Ama kuwafunza watoto au kuwafunza watu wakubwa Qur-aan na mtu akapokea malipo juu yake hakuna neno.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (10) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191426#219753
  • Imechapishwa: 05/05/2019