Swali: Ni ipi hukumu mfungaji akitokwa na damu puani na mfano wake? Je, inajuzu kwa mfungaji kujitolea damu yake na kuchotwa damu kwa ajili ya kipimo?

Jibu: Mfungaji kutokwa na damu, kama puani na damu ya ugonjwa, hakuharibu swawm. Kinachoharibu swawm ni damu ya hedhi, nifasi na damu ya kuumikwa (chuku).

Hapana ubaya kwa mfungaji kuchotwa damu kwa ajili ya kipimo wakati wa kuhitajia kufanya hivo. Hilo haliharibu swawm.

Ama mtu kujitolea damu lililo salama zaidi ni yeye kuchelewesha hilo mpaka baada ya kukata swawm. Kwa sababu mara nyingi inakuwa damu nyingi. Hiyo kunafanana na kufanyiwa chuku.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (15/273)
  • Imechapishwa: 29/05/2018