Ni lazima alipe kabla ya Ramadhaan ya pili?

Swali: Kuna mwanamke dhaifu alikula katika Ramadhaan siku saba, na kwa sasa hawezi kuzilipa. Je, atafunga kabla ya Ramadhaan inayokuja au wakati wowote autakao?

Jibu: Ukiweza kufunga kabla ya Ramadhaan fanya hivyo, isipokuwa ikiwa atakuwa ni mwenye udhuru atafunga baada ya Ramadhaan. Lakini ikiwa ni baada ya Ramadhaan atafunga na kulipa kafara kwa kila siku moja kumlisha masikini. Ikiwa alikuwa hana udhuru wa kuchelewesha. Kama alikuwa na udhuru kwa kuchelewesha atalipa tu.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Waswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://alwasabi.al3ilm.com/alfatawaa
  • Imechapishwa: 10/05/2020