Swali: Je, asali inatolewa zakaah? Ni kipi kiwango chake na kipimo chake? Kwa sababu nyuki zimekuwa nyingi siku hizi. Je, kinachotolewa ni asali yenyewe au pesa?

Jibu: Maoni sahihi ni kuwa asali haitolewi zakaah. Hilo halikuthibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kujengea juu ya hili sio wajibu asali kuitolea zakaah. Lakini mtu akitoa kwa ajili ya usalama zaidi ni jambo la kheri na huenda ikawa ni sababu ya nyuki na asali yake kuwa nyingi. Ama kusema kwa kukata moja kwa moja ya kwamba mtu anapata dhambi kwa kuacha kutoa ni jambo halina dalili.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (05)
  • Imechapishwa: 02/05/2020