Je, Allaah (´Azza wa Jall) anasifiwa kuwa yupo?


Swali: Je, Allaah (´Azza wa Jall) anasifiwa kuwa yupo (الموجود)?

Jibu: Hapana. Kunaelezwa kuhusu Allaah ya kwamba yupo. Sifa ni kwa mujibu wa dalili (توقيفية). Mlango wa maelezo ni mpana zaidi kuliko mlango wa sifa. Kunaelezwa juu Yake ya kwamba yupo, kwamba ni dhati na kwamba ni kitu. Amesema (´Azza wa Jall):

قُلْ أَيُّ شَيْءٍ أَكْبَرُ شَهَادَةً ۖ قُلِ اللَّـهُ ۖ شَهِيدٌ بَيْنِي وَبَيْنَكُمْ

“Sema: “Ni kitu gani ushahidi wake ndio mkubwa zaidi? Sema: “Allaah; ni Mwenye kushuhudia yote kati yangu na kati yenu.”[1]

Hakusemwi kwamba miongoni mwa majina Yake ni dhati, kitu na kuwepo. Aidha kunaelezwa juu Yake ya kwamba ni mzungumzaji. Hakusemwi kwamba miongoni mwa majina Yake ni mzungumzaji (المتكلم). Kwa sababu hakukupokelewa jambo hilo.

[1] 06:19

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (23)
  • Imechapishwa: 28/01/2022