Je, alama ya Sujuud usoni ni dalili kwamba mtu ni mwema?

Swali: Je, kumepokelewa chochote juu ya kwamba ile alama inayosababishwa na kusujudu sana kwenye paji la uso kwamba ni miongoni mwa alama za waja wema?

Jibu: Hii sio miongoni mwa alama za waja wema. Ni nuru tu inayokuwa usoni, kukunjuka kwa kifua, tabia njema na mfano wa hayo. Kuhusu athari inayosababishwa na Sujuud usoni wakati mwingine inaweza kuonekana kwenye nyuso za wale ambao hawaswali isipokuwa tu swalah za faradhi kutokana na ulaini wa ngozi. Sambamba na hilo kuna uwezekano isionekana kwenye nyuso za wale wanaoswali zaidi ya hivo na pia wanarefusha Sujuud zao.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Arkaan-il-Islaam, uk. 329
  • Imechapishwa: 09/05/2020