Swali: Mtu akikidhi haja kubwa au haja ndogo kisha akatamba kwa mawe kisha akatokwa na josho – je, kijasho hiki kinanajisi mavazi?

Jibu: Ni lazima wakati wa kutamba kwa mawe kusafisha. Akihakikisha kuwa amejisafisha kwa mkojo au kinyesi basi jasho hiyo hainajisi yale maeneo yaliyogusana na nguo. Kwa sababu usafishaji aliyofanya mahali pale unazingatiwa kuwa ni pasafi.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy

´Abdullaah bin Ghudayyaan

´Abdullaah bin Qu´uud

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah nr. (9040)
  • Imechapishwa: 09/06/2022