Janga kusema kuwa Ibliys alikuwa muislamu


Swali: Wako wenye kusema kuwa Ibliys hakukufuru kwa sababu alisema:

رَبِّ

”Mola!”[1]

فَبِعِزَّتِكَ

”Naapa kwa utukufu Wako.”[2]

Kwa msemo mwingine ni mwenye kutambua utukufu na ubwana wa Allaah.

Jibu: Ndio, ni mwenye kutambua Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah. Abu Jahl na Abu Lahab, ambao ni makafiri na wataingia Motoni, walikuwa ni wenye kutambua Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah kwa sababu walikuwa ni wenye kukanusha Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah. Ibliys alikataa kutekeleza amri ya Mola wake. Alimwasi Mola wake na akafanya jeuri:

إِلَّا إِبْلِيسَ أَبَىٰ وَاسْتَكْبَرَ وَكَانَ مِنَ الْكَافِرِينَ

”… isipokuwa Ibliys alikataa na akatakabari na akawa miongoni mwa makafiri.”[3]

Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah haitoshi na kusema tu:

رَبِّ

”Mola!”

فَبِعِزَّتِكَ

”Naapa kwa utukufu Wako.”

Hilo halitoshi. Ikiwa kweli kuna ambaye anasema kuwa Ibliys alikuwa muislamu basi ni msiba. Huo ni msiba.

[1] 15:31

[2] 38:82

[3] 02:34

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://alfawzan.ws/node/1875 Tarehe: 1431-04-14/2010-03-29
  • Imechapishwa: 24/01/2021