Jamhuri ya Ummah inathibitisha maneno yaliyosimama katika nafsi ya Allaah?


Halafu al-Khaliyliy akazungumzia kuhusu maneno yaliyosimama ndani ya nafsi na akasema kuwa Mu´tazilah wanapinga hilo na akathibitisha kuwa Ibaadhiyyah na Ashaa´irah wanayathibitisha. Halafu akasema kuwa jamhuri ya Ummah wanayathibitisha. Tazama katika kitabu chake hichi, ukurasa wa 105.

Madai ya kwamba jamhuri ya Ummah inaonelea kuwa maneno ya Allaah yamesimama katika nafsi Yake ni madai batili na yasiyokuwa na dalili yoyote. Wanachuoni wa Salaf wa Ummah huu na waliokuja nyuma wanaraddi yale yanayoitwa ´maneno yaliyosimama katika nafsi`. Kitu cha sampuli hii hakizingatiwi kuwa ni maneno na wala hayapelekei katika hukumu yoyote. Mjadala na al-Khaliyliy katika kuraddi yaliyokuja katika utangulizi wake chini ya kichwa cha khabari “Munaaqashat-ul-Khaliyliy fiy Kalaam-in-Nafsiy”, uk. 161 na nikayaponda maneno yake. Miongoni mwa dalili zake ni kuwa anatumia hoja mashairi ya mnaswara ambaye ni al-Akhtwal. Hakuna haja ya kuyarudi.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd al-Qawiym, uk. 191-192
  • Imechapishwa: 14/01/2017