al-Marruudhiy amesema:

“Nilipokea barua kutoka pande za Shiraaz ambayo ndani yake kulikuwa kumeandikwa kwamba imani zimeumbwa. Waliposikia hivo wakamfukuza nje ya mji.”

Haya ni miongoni mwa mambo yenye kuzidi juu ya haja na vyema zaidi ni kuyanyamazia. Yaliyosihi kutoka kwa Salaf na wanachuoni ni kwamba imani ni maneno na vitendo. Hapana shaka yoyote kwamba matendo yetu yameumbwa kwa sababu Allaah (Ta´ala) amesema:

وَاللَّـهُ خَلَقَكُمْ وَمَا تَعْمَلُونَ

“Ilihali Allaah amekuumbeni pamoja na vile mnayoyafanya.”[1]

Kwa hiyo baadhi ya mambo ya imani yameumbwa. Kusema kwetu ´hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah` kunaingia katika imani yetu na utamkaji wetu pia umeumbwa. Ama kuhusu neno lenyewe halikuumbwa kwa sababu limetoka ndani ya Qur-aan. Allaah atulinde kutokamana na fitina na matamanio.

[1] 37:96

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (12/407-408)
  • Imechapishwa: 29/11/2020