Swali: Yapi maoni yako kwa mwenye kusema: “Ikiwa kutoka na Jamaa´at-ut-Tabliygh ni Bid´ah, basi kutafuta elimu ni Bid´ah.”

Jibu: Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Anasema kumwambia Mtume Wake Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

وَقُل رَّبِّ زِدْنِي عِلْمًا

“Na sema (uombe): “Mola wangu! Nizidishie elimu”.”(20:114)

أَفَمَن يَعْلَمُ أَنَّمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ الْحَقُّ كَمَنْ هُوَ أَعْمَىٰ ۚ إِنَّمَا يَتَذَكَّرُ أُولُو الْأَلْبَابِ

“Je, anayejua kwamba yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Mola wako ni haki (akayafuata, je, ni sawa) kama aliyekuwa kipofu? Hakika wanazingatia wenye akili (tu).” (13:19)

يَرْفَعِ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَالَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ دَرَجَاتٍ

“Atawainua wale walioamini miongoni mwenu na waliopewa elimu daraja (za juu).” (58:11)

إِنَّمَا يَخْشَى اللَّـهَ مِنْ عِبَادِهِ الْعُلَمَاءُ

“Hakika wanaomkhofu Allaah (kikweli kweli) miongoni mwa waja Wake ni Ma’ulaamaa.” (35:38)

Watu hawa wanaosema maneno kama haya ni wenye jeuri. Ama Jamaa´at-ut-Tabliygh, wao ni Bid´ah. Jamaa´at-ut-Tabliygh wao wenyewe ni Bid´ah enyi ndugu zangu. Kwa nini? Kusoma siku arubaini, Taswawwuf na Madu´aat wajinga. Wanasema msijifunze elimu. Wanasema kuwa hakuna kitu kimewaweka mbali wanachuoni na kutokulingania isipokuwa ni elimu. Mmsema uongo, mmsema uongo. Kitu ambacho kimewaweka mbali baadhi ya wanachuoni na kutokulingania ni kazi na dunia, ama kusema kuwa ni elimu hapana si kweli. Hakika ya Allaah (´Azza wa Jalla) Anasema katika Kitabu Chake Kitukufu:

وَلْتَكُن مِّنكُمْ أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى الْخَيْرِ

“Na uweko (watokeze) kutoka kwenu Ummah unaolingania kheri.” (03:104)

Hebu wacha niwaulize: “Je, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa ni mwanachuoni au hakuwa ni mwanachuoni”? Ni jambo lisilokuwa na shaka yoyote ya kuwa jawabu ni kwamba alikuwa ni mtu mjuzi zaidi kumjua Mola Wake. Kama Alivyosema yeye mwenyewe (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Ikiwa hali ni namna hiyo, je elimu ilimuweka mbali na kutokufanya Da´wah? Hapana, elimu haikumuweka mbali na kukosa kufanya Da´wah na Jihaad katika njia ya Allaah. Na nyiyni (Jamaa´at-ut-Tabliygh) ni kitu gani ambacho kimewaweka mbali na kupigana Jihaad katika njia ya Allaah? Mmeng´ang´ania tu kutoka kufanya Da´wah katika njia ya Allaah. Mnatoka na kurejea na huku mmejaribiwa kwa Bid´ah. Na wale wanaotoka nao, wakuta mmoja wao anatoka na kubaki nje miaka nne naye bado angali juu ya Bid´ah zake. Mimi simnasihi yeyote kutoka nao. Da´wah yao ni Bid´ah na wao wenyewe ni Bid´ah. Ama kutoka na kutafuta elimu, mmedanganya ikiwa mtasema kuwa ni Bid´ah. Sioni mwingine aliyesema hivi ila ni mjinga wakutupilia. Vipi mnaweza kusema kuwakutafuta elimu ni Bid´ah hali ya kuwa elimu huzingatiwa kuwa ni nuru na wanachuoni wao ndio wanayaweka mambo mahala pake panapostahiki. Allaah (Ta´ala) Anasema:

وَمَا يَعْقِلُهَا إِلَّا الْعَالِمُونَ

“Hawaifahamu isipokuwa wenye elimu.” (29:43)

إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّلْمُؤْمِنِينَ

“Hakika katika hayo ni Aayah kwa Waumini.” (15:77)

فَخَرَجَ عَلَىٰ قَوْمِهِ فِي زِينَتِهِ ۖ قَالَ الَّذِينَ يُرِيدُونَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا يَا لَيْتَ لَنَا مِثْلَ مَا أُوتِيَ قَارُونُ إِنَّهُ لَذُو حَظٍّ عَظِيمٍ وَقَالَ الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ وَيْلَكُمْ ثَوَابُ اللَّـهِ خَيْرٌ لِّمَنْ آمَنَ وَعَمِلَ صَالِحًا وَلَا يُلَقَّاهَا إِلَّا الصَّابِرُونَ

“Basi akawatokea watu wake katika pambo lake. Wakasema wale wanaotaka (wanaopendelea na kufadhilisha) maisha ya dunia wakasema: “Ee laiti tungelipata mfano wa yale aliyopewa Qaaruwn, hakika yeye ana bahati kubwa mno.” Na Wakasema wale waliopewa elimu: “Ole wenu! Thawabu za Allaah (Aakhirah) ni bora zaidi kwa yule aliyeamini na akatenda mema. Na wala hazipati isipokuwa wenye kusubiri.” (28:79-80)

Muhimi ni kuwa, hii ni kauli ya kiwani. Sio kauli ya mwanaume, ni kauli ya kiwani enyi ndugu zetu. Ni sahihi kwa yule mwenye kusema ya kwamba kujifunza elimu ni Bid´ah, ni kiwani na wala haitakikani kuzingatiwa wala kurejelewa (kuchukua elimu kwake).

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=rQ_TJbBEPt4
  • Imechapishwa: 21/03/2018