Swali: Ni ipi hukumu ya kusafiri kwa kukhusisha siku tatu au siku arubaini kwa ajili ya Da´wah?

Jibu: Da´wah isiwekewe kiwango cha masiku maalum. Hili halina dalili yoyote. Ni Bid´ah. Mtu asiweke kiwango.

Mtu atoke ikiwa uko na elimu. Kuhusu mjinga hatakiwi kutoka kwa ajili ya Da´wah. Ikiwa uko na elimu na unaweza kuwalingania watu katika dini ya Allaah toka pasi na kuweka kiwango cha masiku, miezi na kadhalika. Haya ni Bid´ah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13398
  • Imechapishwa: 27/04/2018