Jamaa´at-ut-Tabliygh Wana Mambo Ya Ukhurafi, Bid´ah Na Shirki


Swali: Ni yapi maoni yako kuhusu Jamaa´at-ut-Tabliygh na wana ´Aqiydah sahihi na wanaingia katika Hadiyth ya mapote sabini na mbili [yatayoingia Motoni]?

Jibu: Ndugu zangu! Shaykh Ibn Baaz ameshawajibu juu ya swali hili. Amewajibu kuhusu al-Ikhwaan al-Muslimuun na kuhusu Jamaa´at-ut-Tabliygh. Jamaa´at-ut-Tabliygh wana ukhurafi, Bid´ah na shirki. Mtu asitoke nao isipokuwa mwanachuoni tu anayetoka nao ili awatoe katika upotevu wao na kuwapeleka katika uongofu. Nini mnachotaka?

Ibn Baaz aliwafanyia upole na ulaini kwa muda mrefu. Wakati alipoona wanatumia ulaini na upole, akawapa kipigo kibaya. Allaah Amrahamu. Alifanya hivi mwishoni mwa uhai wake. Tendeeni kazi Fataawaa hizi.

Kadhalika al-Ikhwaan al-Muslimuun. Aliulizwa kuhusu wao kwenye mkanda na akajibu kwenye gazeti na akabainisha kuwa wamepinda. Wao na Jamaa´at-ut-Tabliygh ´Aqiydah zao ni moja: Ash´ariyyah, Suufiyyah, kupetuka mipaka na kukusanya. Mfumo na ´Aqiydah yao ni moja.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=26874
  • Imechapishwa: 19/05/2015