´Iyd ina Khutbah moja au mbili?

Swali: Je, ´Iyd ina Khutbah moja au mbili?

Jibu: Sunnah katika ´Iyd ni kutoa Khutbah moja. Ni sawa pia iwapo kutatolewa Khutbah mbili. Kwa sababu hili limepokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Lakini hata hivyo haitakiwi kupuuzia Khutbah ya wanawake peke yao. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwatolea Khutbah.

Ikiwa kunatolewa kupitia kipaza sauti ambapo wanawake wanasikia, basi inatakiwa vilevile kufanywe Khutbah nyingine ya mawaidha maalum kwa wanawake. Ikiwa hatoi kupitia kipaza sauti na wanawake wakawa hawasikii, basi anatakiwa kwenda kwao. Anatakiwa awe pamoja naye mwanaume mmoja au wawili na azungumze nao kwa kile kitachokuwa rahisi kwake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (16/248)
  • Imechapishwa: 14/06/2018