´Iyd ina Khutbah moja au mbili? II

Swali: Je, Khutbah ya ´iyd ni moja au mbili? Ni ipi dalili ya hilo?

Jibu: Khutbah ya ´iyd ni mbili atatoa Khutbah mbili kama vile ijumaa. Hivi ndivo walivosema wanazuoni. Wamelinganisha ´iyd na ijumaa. Imepokelewa katika baadhi ya Hadiyth zinazofahamisha kuwa Khutbah ya ´iyd ni moja. Lakini katika cheni ya wapokezi wake kuna unyonge. Kinachotegemea katika hayo ni kwamba Khutbah ya ´iyd ni kama ya ijumaa. Kwa sababu ni sikukuu ya mwaka na ijumaa ni sikukuu ya wiki. Kwa hivyo wanazuoni wamelinganisha swalah ya ´iyd juu ya swalah ya ijumaa. Atatoa Khutbah mbili.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/10698/ادلة-خطبتي-العيد
  • Imechapishwa: 30/04/2022