Swali: I´tikaaf huanza lini?

Jibu: Wanachuoni wengi wanaonelea kuwa I´tikaaf inaanza usiku wa kuamkia tarehe 21 na sio alfajiri ya tarehe 21. Lakini hata hivyo wapo wanachuoni wenye kuonelea kuwa I´tikaaf inaaza alfajiri ya tarehe 21 wakitumia dalili Hadiyth ya ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) iliyopokelewa na al-Bukhaariy isemayo:

“Aliposwali Fajr ndipo akaingia katika I´tikaaf yake.”

Lakini wanachuoni wengi hao wamejibu ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) asubuhi hiyo alikuwa peke yake na hakuwa na watu. Kuhusu nia ya I´tikaaf ni katika ule usiku wa kwanza. Yale masiku kumi ya mwisho yanaanza kuanzia pale jua linapozama siku ya ishirini.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (20/169-170)
  • Imechapishwa: 21/06/2017