I´tikaaf dakika kadhaa kwa anayesubiri swalah

Swali: Mtu akiingia msikitini kwa takriban dakika 10 au 15. Je, inafaa kwake akanuia I´tikaaf?

Jibu: Akinuia hapana vibaya. Kwa hali yoyote yuko kwenye ´ibaadah. Ni mamoja amenuia au hakunuia I´tikaaf. Analipwa thawabu kwa kukaa na kusubiri kwake. Anayesubiri swalah yuko ndani ya swalah. Malaika wanamuombea du´aa na msamaha. Ni sawa pia akinuia I´tikaaf.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22844/هل-تشرع-نية-الاعتكاف-لمن-دخل-المسجد
  • Imechapishwa: 08/09/2023