Istighfaar ni sababu ya kupata riziki

Swali: Kufanya istighfaar ni miongoni mwa sababu za kupata riziki?

Jibu:

وَمَن يَتَّقِ اللَّـهَ يَجْعَل لَّهُ مَخْرَجًا وَيَرْزُقْهُ مِنْ حَيْثُ لَا يَحْتَسِبُ

“Na yeyote yuleanayemcha Allaah, atamjaalia njia [ya kutoka katika matatizo] na atamruzuku kutoka njia ambayo hatizamii.” (65:02-03)

Kufanya istighfaar na kuomba msamaha ni katika kumcha Allaah.

Swali: Mtu akusanye Dhikr na kufanya istighfaar vyote kwa pamoja?

Jibu: Ndio, mara afanye hivi na mara afanye hivi. Mara amtaje Allaah na mara nyingine afanye istighfaar.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22734/هل-الاستغفار-من-اسباب-الرزق
  • Imechapishwa: 12/08/2023
Takwimu
  • 325
  • 373
  • 1,819,093