Swali: Je, wale wenye kujiita “ISIS” wanahesabika ni ukhaliyfah mwongofu wa Kiislamu?
Jibu: Hapana, sio ukhalifah mwongofu wa Kiislamu. Ukhaliyfah mwongofu unahakikishwa na wanachuoni wakubwa wa Kiislamu na waislamu wakubwa wenye akili wanaolisoma suala kati yao na kisha wanamteua mtawala ikiwa hajakuwa na utawala.

Kuhusiana na wale wenye kujiita ISIS na wengine, matendo yao ni fitina na kuchochea shari. Allaah peke Yake ndiye anayejua ikiwa kama hawa hawatumiwi na maadui wa Uislamu ili ujinga juu Uislamu na [sauti haisikiki] uenee. Haijuzu kwa yeyote kusafiri ili kujiunga na ISIS na watu mfano wao. Si halali kwake.

  • Mhusika: ´Allaamah Swaalih bin Muhammad al-Luhaydaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=149597
  • Imechapishwa: 06/11/2016