ISIS ni vile vitu vya michezo wanavyochezea watoto

Swali: Kuna vijana ambao wamedanganyika na ukhalifah unaodaiwa ambao umetangazwa Syria na ´Iraaq. Ni ipi nasaha yako kwao?
Jibu: Enyi Waislamu! Watu hawa ni Khawaarij wenye mfumo na fikira alizotahadharisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wana uovu na ufisadi unaojua Allaah peke Yake.

Wanachuoni wameandika na kuzungumza sana na kwa undani kuhusiana na mapote haya kwa ujumla na khaswa pote hili. Wakweli, wasokuwa na makundi na wajuzi wanaona ni uovu na ufisadi gani unaopatikana katika kundi hili. Wao ni sababu ya maadui wa Uislamu kuwashinda Waislamu. Wao ni sababu ya Waislamu kupatwa na madhara. Ni fitina, shari, ufisadi, ukandamizaji na uadui kiasi gani wamesababisha katika nchi za Kiislamu! Kumepokelewa mapokezi sahihi kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Wanawaua waislamu na wanawaacha washirikina.”

Mnajua kipi kilichofanywa na kundi hili hivi karibuni. Baya kuliko hilo ni kwamba wanawadanganya Waislamu wengi wajinga na kuwatupa katika fitina hizi. Kwa masikitiko makubwa kuna wengi wanaowafosi vijana wakati wao wenyewe wamejiweka mbali. Kwa nini wewe usiende pamoja nao ikiwa kama kweli ni wapigana Jihaad walioko katika haki? Kwa nini wewe usimtume mtoto wako? Unawaunguza watoto wa Waislamu na unawahamasisha na kuwafosi ukiwa mbali. Pindi mmoja wao anapoathirika hatahadharishi na pote hili potevu. Huenda akasema kuwa hajabainikiwa na mambo, vyombo vya khabari vinadanganya sana, wanaweza kuwa wamedhulumiwa na maneno mengine ya utatizi. Haya pamoja na kwamba kumethibitishwa uovu na ufisadi mwingi wa kundi hili potevu.

Mnajua pia jinsi pote hili lilivyoeneza uovu na ufisadi sehemu nyingi. Wanadai kuwa wanaunusuru Uislamu na Waislamu. Uislamu haunusuriwi kwa batili. Uislamu haunusuriwi kwa fikira hizi za kipotevu, Takfiyr, malipuaji, kuhalalisha ya haramu na kuwashambulia Waislamu. Bali huu ndio mfumo wa Khawaarij ambao Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitahadharisha.

Hakuna mwanachuoni yeyote kati yao. Hakuna mwanachuoni yeyote anayejulikana anayewasapoti. Yaliyotajwa katika baadhi ya mapokezi yanaafikiana na wao:

“Wadogo kiumri na ni wapumbavu wa akili.”

Hizi ndio sifa na hali zao.

Lau Waislamu wangelirejea kwa ukweli na inswafu kwa wanachuoni wakubwa wenye kujulikana kuwa na uaminifu na dini, wangelijua kuwa watu hawa ni wapotevu na kwamba dini inachukuliwa kutoka mahala pake sahihi. Unapohitajia kujua kitu fulani katika ´Aqiydah na ´ibaadah usiwaulize watu hawa. Unajua ni kina nani utaowauliza. Tafuta wanachuoni walezi kama al-Lajnah ad-Daaimah, Shaykh Ibn Baaz, Shaykh Ibn ´Uthaymiyn na wanachuoni na maimamu wengine wa leo na waliowatangulia. Kwa nini katika suala hili wasirejelewe wanachuoni hawa? Mnarejea kwa watu wasiojulikana wanaozungumza nyuma ya pazia. Hujui ni nani anayezungumza au kutoa fatwa. Wanawahamasisha vijana kwa hisia na hamasa.

Kwa ajili hii ndio maana ni lazima kwetu Waislamu kujua kuwa dini ya Allaah haikujengwa juu ya maoni, matamanio, hisia wala hamasa. Imejengwa juu ya hoja na dalili. Watu hawa si jengine isipokuwa ni vitu vya kuchezea vya bandia (puppets). Maadui wa dini wanawatumia ili kufikia malengo yao. Ni makundi mangapi na dola za uogo, za kudaiwa na za kindoto zimekuja na kwenda! Walionekana tu kama vitu vya kuchezea vya bandia vya maadui kwa malengo yao kisha vinatupwa katika taka. Mwisho wake nafsi nyingi tu ndio hupotea pasina faida na vijana wengi wanaotumbukia kwenye muhanga wa fitina hii.

Hivyo basi, hatupati mazingatio, kuelewa na kufahamu ya kwamba matukio kama haya hayawasababishii Waislamu jengine isipokuwa khasara na madhara na kwamba unusuriwaji wa Uislamu unakuwa kwa kushikamana tu na Qur-aan na Sunnah na kuvitendea kazi na pindi watu wanapokuwa wamekusanyika kwa wanachuoni Rabbaaniyyuu?

  • Mhusika: Shaykh ´Abdullaah bin ´Umar al-´Adniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=69vx3F5dTxI&app=desktop
  • Imechapishwa: 07/02/2017