Swali: Tunaona jinsi Magharibi hatimaye wameanza kutishia kuingia Iraaq. Kwanza ISIS waliua na kuteka nyara. Wakati walipoanza kuwaua wanaume wa kinaswara na kuwafunga wanawake wao Magharibi ikajiingiza.

Jibu: Sababu ni ipi? Tunaligeuza swali na kuuliza ni nani aliyesababisha hili. Je, si hawa Takfiyriyyuun ndio walioanza kuwaua Waislamu, licha ya manaswara? Wanamuua kila mwenye kwenda kinyume na wao na wanamchinja kama kondoo. Wanawaua watoto, wazee na wanawake wa Kiislamu. Ni nani aliyowatakasia hawa makafiri wa mashariki na wa magharibi kuwavamia Waislamu kwa sababu ya matendo yao machafu:

وَمَا أَصَابَكُم مِّن مُّصِيبَةٍ فَبِمَا كَسَبَتْ أَيْدِيكُمْ وَيَعْفُو عَن كَثِيرٍ

Na haukusibuni katika msiba wowote ule, basi ni kwa sababu ya yale yaliyochuma mikono yenu, na Anasamehe mengi.” (42:30)

Ni hawa Takfiyriyyuun na Khawaarij ndio ambao wamewafanyia njia hawa makafiri kwa matendo haya. Hivi sasa Syria wanashirikiana na Nusayriyyah dhidi ya Ahl-us-Sunnah. Wanafanya kadhalika Iraaq na sehemu zingine. Wanashirikiana na maadui wa Ahl-us-Sunnah kati ya Raafidhwah na wengineo wakati wanadai kuwa ni maadui wa watu hawa. Wamewaua Ahl-us-Sunnah wengi Iraaq zaidi kuliko Raafidhwah. Wote wana madhehebu yasiyokuwa salama; Raafidhwah na Khawaarij. Haijalishi kitu ni mwelekeo gani walonao na haijalishi kitu wanaitwa kwa majina yepi. Ni jambo lisilokuwa na shaka ya kwamba wote wako upotevuni na wametoka katika Uislamu:

لَا يَرْقُبُونَ فِي مُؤْمِنٍ إِلًّا وَلَا ذِمَّةً ۚ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُعْتَدُونَ

Hawachungi kwa Muumini udugu [wa damu] wala dhima [ya himaya]. Na hao ndio wapindukao mipaka.” (09:10)

Ni nani aliyewafanyia njia? Ndio, ni watu wenye kutoa Fatwa potevu. Wamewapoteza vijana wetu mbali na sarabi. Wamewaahidi msamaha kama wanavofanya manaswara na mapadiri. Wanawaambia kuwa wanawake wa Peponi wamesimama na kuwasubiri wakijilipua sehemu fulani.

Jambo la ajabu ni kwamba huwezi kusikia wanazungumza juu ya kulinyanyua neno la Allaah na kuinusuru Dini. Wanaimba tu na kupiga kelele na kila kitu kinahusiana tu na wanawake wa Peponi. Bila ya shaka wanawake wa Peponi ni katika neema za Peponi. Ni haki na kila Muislamu anatamani hilo, lakini kila kitu kuhusiana na hilo huu ni ujinga.

Nilimuuliza mmoja wao katika kundi la majadiliano kama ameoa. Akaapa kwa Allaah kwamba ni wakati mdogo tu ndio ulipita kati yake yeye na kuoa. Wakati nilipomuomba anifafanulie, akasema:

“Ningelioa wanawake wa Peponi badala ya kuoa wanawake wa udongo. Lakini walinizuia pindi waliponikatama.”

Nikamwambia amshukuru Allaah kwa kukamatwa na kumwacha akaenda kuua, kuuawa, kuudhi au kuudhiwa. Nikamwambia amshukuru Allaah ambaye Amemuokoa na kwenda kuwaua Waislamu kwa kutumia jina la udanganyifu la Jihaad. Ni udajali. Sio Jihaad. Ni ufisadi. Waangalie watu hawa.

Jana Khawaarij hawa wameua watu 150 wa Ahl-us-Sunnah Iraaq. Mara moja. Hatuhitajii kuingia kwa undani ni njia gani ya kutisha wanayotumia katika kuwaua. Masiku kadhaa ya nyuma wameua watu watano. Ni wachaji Allaah, Mashaa Allaah! Wanawaambia watamke Shahaadah. Wakati wanapotamka Shahaadah wanawaua. Mmeyatoa wapi haya? Kwa nini unamuua mtu ambaye umemuamrisha kutamka Shahaadah na baada ya hapo amefanya hivo na kuingia katika Uislamu? Kwa nini unamuua? Jibu lao ni kwamba wanataka wafe wakiwa ni Waislamu. Anatamka Shahaadah kwanza, kisha wanamchinja kama kondoo.

Watu hawa ni wabaya. Inavyoonekana – na Allaah ndiye Anajua zaidi – ni kwamba wamepandwa na makafiri, sawa ikiwa wanajua hilo au hawajui.

Jana kuna mwanamke alikuwa ananadi:

“Shaykh al-Baghdaadiy! Jiunge na sisi! Watoto wetu wameenda! Watoto wetu wamefungwa! Watoto wetu hili na lile!”

Huyu ni mwanamke anayeishi katika neema. Mwanamke anayeishi katika sitara. Anaishi katika nchi ya amani na nchi ya sitara. Anataka kujiunga na wapumbavu hawa. Anawaandikia kwenye Twitter. Anataka wamuokoe kutoka kwenye nchi ya Kiislamu na kujiunga na watu hawa wenye kutoka katika Dini ya Allaah (´Azza wa Jalla). Kuweni hange! Muislamu asiwe mshenzi na mpumbavu. Rejea kwa wanachuoni Rabbaaniyyuun[1] na waulize juu ya mambo haya. Ninakuonya na kudanganyika.

Ndugu! Ninaapa kwa Allaah ya kwamba nilipitia jambo lingine katika kundi la majadiliano. Kundi la wanaume lilirudi kutoka katika miji ya fitina. Allaah Aliwatunukia Baswiyrah na uelewa. Wametueleza kitu cha ajabu. Wamesema kuwa kuna kundi lililo na viongozi watatu. Kiongozi wa kwanza yuko huku kwetu. Yeye ndiye mwenye kuwaendesha. Kiongozi mwingine yuko Syria. Kiongozi mwingine yuko Uturuki. Wakati mmoja wao alipowapa kiapo cha usikivu na utiifu na akaenda pamoja nao wakamuuliza ni pesi kiasi gani alizo nazo. Anasema kuwa aliuza gari yake kwa pesa 20.000 SAR. Hivyo wakamwambia abaki na 5000 SAR na atoe 15.000 SAR kuwapa wateja wa ndani ili kununua silaha za kupigania. Anaeleza kuwa alipofika huko hakuona Jihaad yoyote. Alichoona tu ni watu wanapigana wao kwa wao. Walimwamrisha kwenda sehemu fulani na kujilipua. Isitoshe sehemu hiyo ilikuwa mji wa Ahl-us-Sunnah. Watu huko walikuwa ni Ahl-us-Sunnah. Wakati alipojaribu kujadiliana nao kuna mtu alimnong´oneza (ambaye yeye mwenyewe alidanganywa huko na anataka kurudi) ya kwamba watamuua lau atawaasi. Ukiweza kurudi nyumbani kwenu fanya hivo. Mimi mwenyewe najaribu kufanya hivo. Alijaribu kufanya hivo kwa miezi miwili, lakini alitishwa kuuawa lau atatikisika.

Ndugu! Mambo haya yanakariri mara kwa mara. Tahadharini na kuweni hange. Watahadharisheni watoto zenu kusikiliza Fataawa hizi potevu zinazotoka kwa watu hawa wapotevu. Waamrisheni kurejea kwa wanachuoni Rabbaaniyyuun ambao wanakilinda Kitabu cha Allaah dhidi ya mabadilisho ya wapetukaji, maneno ya waongo na tafsiri za kimakosa za wajinga.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin Sa´d as-Suhaymiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=146354
  • Imechapishwa: 09/04/2015