ISIS Ni Kundi La Kishaytwaan


ISIS na kila anayepinda kutokamana na njia iliyonyooka ni katika pote la Shaytwaan; ima ni katika Khawaarij au wengine katika wanaofanya propaganda ya upotevu. Hawawezi kukabidiliwa isipokuwa kwa elimu yenye manufaa. Ni katika wale ambao Allaah amesema juu yao:

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ جَاهِدِ الْكُفَّارَ وَالْمُنَافِقِينَ وَاغْلُظْ عَلَيْهِمْ ۚ وَمَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ ۖ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ

“Ee Nabii! Pambana Jihaad na makafiri na wanafiki na kuwa mgumu kwao; na makazi yao ni Motoni – na ubaya ulioje mahali pa kuishia!” (09:73)

Wanatumbukia katika safu ya wanafiki kwa kuwa wanadai Uislamu wanatendea kazi baadhi ya nembo za kidini. Pamoja na hivyo ni walinganizi wa kipotevu na hawawezi kukabiliwa isipokuwa kwa elimu yenye manufaa na kuraddi utata na batili zao.