´Ishaa ya sura hii kwa msafiri haisihi


Swali: Msafiri akitaka kuswali ´Ishaa kwa kufupisha akakutana na mkusanyiko wanaswali Maghrib ambapo akasubiri mpaka walipomaliza Rak´ah ya kwanza kisha ndio akajiunga nao na akatoa Tasliym pamoja nao. Je, kitendo hichi kinafaa?

Jibu: Swalah hii haisihi. Katika hali kama hii ni lazima kwake kuirudi na amfuate imamu. Swalah ikiwa ni yenye kutofautiana; ya Rak´ah tatu na Rak´ah nne, basi itambulike kuwa wanachuoni wametofautiana. Baadhi yao wanaona kuwa aswali pamoja nao na aketi. Wanachuoni wengine wanaona kuwa haisihi na bali anatakiwa kuiswali kwa kunuia kuwa ni swalah ya sunnah. Kisha baada ya hapo ndio aswali faradhi. Kwani ni swalah mbili zenye kutofautiana. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika si venginevyo imamu amewekwa ili afuatwe. Hivyo msitofautiane naye.”

Ama ikiwa swalah ya imamu na maamuma ni ya Rak´ah nnenne basi hakuna neno.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (19)
  • Imechapishwa: 21/02/2021