Swali: Mtu anaweza kuoga kwa ajili ya kila swalah au ni wajibu kwa mtu kuoga?

Jibu: Ndio, akinuia wudhuu´ ndani ya uogaji uliyowekwa katika Shari´ah. Uogaji ni lazima uwe uliowekwa katika Shari´ah au sio kwa ajili ya lengo la kutaka kupata baridi au kujisafisha. Kwa mfano uogaji kwa ajili ya siku ya swalah ya Ijumaa au janaba. Akinuia wudhuu´ kuingia ndani yake unaingia. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika kila ´amali inazingatia nia na kila mmoja atalipwa vile alivyonuia.”

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (12) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-08-02.mp3
  • Imechapishwa: 03/06/2018