Inatosha akahukumu au akahukumiwa mara moja tu

Swali 104: Je, kubadilisha Shari´ah ya Kiislamu kwa kanuni zilizotungwa ni kufuru kwa dhati yake au ni jambo linahitajia uhalalishaji wa kimoyo na kuitakidi kujuzu kwa jambo hilo? Je, kuna tofauti kuhukumu mara moja tu kinyume na yale aliyoteremsha Allaah na kuzifanya kanuni kuwa ni Shari´ah iliyoenea pamoja na kuamini kutofaa jambo hilo?

Jibu: Ionekanavyo ni kwamba hakuna tofauti katika suala moja, mara kumi, mara mia, mara elfu moja au chini ya hapo au zaidi ya hapo. Hakuna tofauti. Midhali mtu anajihesabu kuwa ni mwenye kukosea, kwamba amefanya jambo la kimadhambi, kwamba amefanya maasi na ni mwenye kuogopa dhambi, basi hiyo ni kufuru ndogo.

Ama pamoja na uhalalishaji, ingawa itakuwa ni katika suala moja tu, ambapo akahalalisha kuhukumu kinyume na aliyoteremsha Allaah na akaizingatia nafsi yake kuwa ni mwenye kuhalalisha, basi anazingatiwa ni kafiri.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ´Ulamaa-ul-Kibaar fiy al-Irhaab wat-Tadmiyr, uk. 274
  • Imechapishwa: 19/10/2019