Inatakiwa kutanguliza deni kwanza kabla ya swawm ya Shawwaal


Swali: Inajuzu kufunga siku sita za Shawwaal kabla ya mtu kulipa deni lake la Ramadhaan?

Jibu: Wanachuoni wametofautiana katika hilo. Usawa ni kwamba jambo lililowekwa katika Shari´ah ni kutanguliza kwanza deni kabla ya kufunga zile siku sita za Shawwaal na Sunnah nyenginezo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Atakayefunga Ramadhaan kisha akaifuatishia siku sita za Shawwaal basi ni kama ambaye amefunga mwaka mzima.”[1]

Ameipokea Muslim katika “as-Swahiyh” yake.

Atakayetanguliza siku sita kabla ya kulipa hakuifuatishia Ramadhaan. Ameifuatanishia baadhi ya siku za Ramadhaan. Jengine ni kwamba kulipa deni ni faradhi. Kufunga faradhi kuna haki zaidi ya kupewa umuhimu.

[1] Muslim (1164), at-Tirmidhiy (759), Abu Daawuud (2433), Ibn Maajah (1716), Ahmad (05/417) na ad-Daarimiy (1754).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (15/392)
  • Imechapishwa: 09/06/2018