Inatakiwa kuswali kwa kuelekea Sutrah


Swali: Ni katika Sunnah Sutrah kuiweka upande wa kulia, wa kushoto au iwe usawa na yeye mbele yake?

Jibu: Sunnah ni yeye kuswali kwa kuielekea. Kuhusu yale yaliyopokelewa katika baadhi ya Hadiyth kwamba mtu asiikusudie Sutrah na kuwa apinde kutokamana nayo upande wa kulia au wa kushoto ni Hadiyth dhaifu. Maoni ya sawa ni kwamba aswali kwa kuielekea.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (20)
  • Imechapishwa: 27/06/2021