Inaruhusiwa kwa mwanamke kuvaa suruwali ya soksi katika Ihraam?

Swali: Je, inafaa kwa mwanamke kuvaa suruwali ya soksi wakati wa Ihraam?

Jibu: Ni sawa. Maadamu sio ya mapambo na ya dhambi anaweza kuvaa kama kawaida. Isipokuwa kitu kimoja ndio hafai kuvaa: Niqaab na vifuniko vya mikono. Mwanamke anatakiwa kujifunika. Hivyo avae mavazi ya kawaida isipokuwa tu Niqaab na vifuniko vya mikono, haya ndio amekataza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (03) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/muq–14331123.mp3
  • Imechapishwa: 17/06/2015