Inajuzu kwa wafanya kazi kuacha kufunga Ramadhaan?


Swali: Inajuzu kwa wafanyakazi kazi ikiwa mgumu kwao wakaacha kufunga?

Jibu: Ni wajibu kwao kufunga na watake msaada kutoka kwa Allaah (´Azza wa Jall). Yule ambaye anataka msaada kutoka kwa Allaah basi Allaah humsaidia. Katikati ya mchana wakiona kiu kinawadhuru au kiu kikawa ni sababu ya kuwaangamiza ni sawa wakala kwa dharurah. Lakini bora kuliko hili ni wao kupatana na bosi kazi zao katika Ramadhaan wazifanye usiku au sehemu ya kazi hizo wazifanye usiku na zengine mwanzoni mwa mchana au wawepesishiwe masaa ya kazi ili waweze kufanya kazi na kufunga kwa njia nzuri.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/89)
  • Imechapishwa: 31/05/2017