Inajuzu kwa myonyeshaji kuacha kufunga?


Swali 406: Inajuzu kwa myonyeshaji kuacha kufunga? Ni lini anatakiwa kulipa? Je, anatakiwa kulisha?

Jibu: Mnyonyeshaji ikiwa anachelea juu ya mtoto mtoto wake funga kwa njia ya kwamba maziwa yanapungua mpaka mtoto anadhurika, basi ana ruhusa ya kula. Lakini anatakiwa kulipa huko baadaye. Kwa sababu ameshabihiana na mgonjwa ambaye Allaah amesema juu yake:

وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ

“Atakayekuwa mgonjwa au safarini basi atimize idadi katika siku nyinginezo.”[1]

Atatakiwa kulipa punde tu ambapo udhuru utamwondoka. Ima afanye hivo wakati wa majira ya badiri kwa sababu mchana unakuwa mfupi  na mazingira yanakuwa ya baridi. Kama hakujaaliwa kulipa wakati wa majira ya baridi basi alipe mwaka unaokuja.

Kulisha chakula ni kwa yule ambaye kikwazo chake au udhuru wake ni wenye kuendelea na hautarajiwi kuondoka. Mtu mwenye hali hii ndiye anayetakiwa kutoa chakula badala ya kufunga.

[1] 02:185

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Arkaan-il-Islaam, uk. 465
  • Imechapishwa: 07/05/2019