Inajuzu kwa mwanamke kutumia dawa ya kuzuia hedhi katika Ramadhaan?

Swali: Inajuzu kwa mwanamke kutumia dawa ya kuzuia hedhi katika Ramadhaan?

Jibu: Inajuzu kwa mwanamke kutumia dawa ya kuzuia hedhi katika Ramadhaan iwapo madaktari wazoefu na ambao ni waaminifu na wengine mfano wao watathibitisha ya kwamba kitu kama hicho hakimdhuru na wala hakiathiri kifaa cha ujauzito wake. Lakini hata hivyo bora ni yeye kutofanya hivo. Allaah amempa ruhusa ya kutokufunga akijiwa na hedhi katika Ramadhaan na amemuwekea kuyalipa masiku yaliyompita na amemridhia jambo hilo kidini.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (10/150-151)
  • Imechapishwa: 02/06/2017