Inajuzu kwa mwanamke kutembelea makaburi mara moja kwa mwaka?

Swali: Je, inajuzu kwa mwanamke kutembelea kaburi au makaburi kwa mwaka mara moja?

Jibu: Hapana. Haijuzu hata kama itakuwa mara moja kwa miaka elfu moja. Haijuzu kwa mwanamke kutembelea makaburi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewalaani wanawake wenye kuyatembelea makaburi. Haijuzu kwa mwanamke kutembelea makaburi. Haijalishi kitu hata kama itakuwa ni kaburi moja au mara moja tu kwa mwaka au kwa miaka. Haijuzu kwake kufanya hivo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (74) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-10-28.mp3
  • Imechapishwa: 22/08/2020