Inajuzu kwa mwanamke kusafiri pasina Mahram kukiaminika usalama wa njia?


Swali: Ni jawabu lipi kwa anayesema kuwa inajuzu kwa mwanamke kusafiri kwa ndege katika masafa mafupi pasina kuwa na Mahram ikiwa anaamini njia?

Jibu: Huyu anaenda kinyume na maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Sio halali kwa mwanamke anayemwamini Allaah na Siku ya Mwisho kusafiri isipokuwa awe pamoja naye Mahram.”

Hakuwekea hilo vikwazo kwamba awe pamoja na kundi au peke yake. Mtume hakuwekea vikwazo. Hadiyth hii ni kwa jumla. Haikhusishwi isipokuwa kwa dalili.

Vile vile wakati alipokuja mtu na kumuomba idhini Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kutoka kwenda vitani na akamwambia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwa mke wake ameenda kwenda Hajj akamwambia:

“Nenda na uhiji na mwanamke wako.”

Hadiyth hii inapatikana katika “as-Swahiyh”. Ni jambo linalojulikana kuwa mwanamke huyu [katika Hajj] anakuwa na kundi la mahujaji. Pamoja na hivyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakutosheka na hilo. Bali alimrudisha mwanaume huyu na kumwambia ahiji na mwanamke wake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (46) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1432-04-01.mp3
  • Imechapishwa: 16/11/2014