Inajuzu kwa muislamu kuhudhuria jeneza la ndugu yake kafiri?

Swali: Je, inajuzu kuhudhuria jeneza la kafiri kwa ajili ya maslahi kwa mfano mtu asipohudhuria jeneza la ndugu yake kafiri jamaa zake watamkasirikia?

Jibu: Haijuzu kufanya hivi. Haijuzu kwa muislamu kumshaji´isha kafiri au kuhudhuria jeneza lake. Kwa sababu kitendo hichi ni katika kumpenda. Isipokuwa katika hali moja; kama hakuna kafiri wa kumzika. Katika hali hii atamzika. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwamrisha ´Aliy kumzika Abu Twaalib. Ikiwa kafiri hana yoyote wa kumzika waislamu watamzika.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (03) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2106
  • Imechapishwa: 01/07/2020