Inajuzu kwa mfungaji kumbusu mke wake na kucheza nae?


Swali: Inajuzu kwa mfungaji kumbusu mke wake na kucheza nae?

Jibu: Inajuzu kwa mfungaji kumbusu mke wake na kucheza nae. Isipokuwa ikiwa atakhofia kuharibika swawm yake kwa kutokwa na manii. Akijiamini kwa hilo [sawa afanye]. Vinginevyo swawm yake inaharibika. Ikiwa ni mchana wa Ramadhaan basi ni lazima ajizuie na kula na kunywa siku iliyobaki. Ni lazima vilevile kuilipa siku hiyo. Ikiwa sio katika Ramadhaan basi atakuwa ameiharibu swawm yake na si lazima kujizuia na kula na kunywa. Lakini ikiwa swawm yake ni ya wajibu basi itakuwa ni wajibu kwake kuilipa siku hiyo. Ikiwa swawm yake ni ya sunnah hakuna dhambi kwake kwa kutoilipa siku hiyo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (01/355)
  • Imechapishwa: 11/06/2017